Walawi 7:26 - Swahili Revised Union Version Tena msiile damu yoyote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi. Biblia Habari Njema - BHND Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi. Neno: Bibilia Takatifu Popote mtakapoishi, kamwe msile damu ya ndege yeyote wala ya mnyama. Neno: Maandiko Matakatifu Popote mtakapoishi, kamwe msinywe damu ya ndege yeyote wala ya mnyama. BIBLIA KISWAHILI Tena msiile damu yoyote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote. |
Nawe utafanya vivyo hivyo katika ng'ombe wako, na kondoo wako; utamwacha siku saba pamoja na mama yake; siku ya nane utanipa mimi.
Basi, waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Mnakula nyama pamoja na damu yake, na kuviinulia vinyago vyenu macho yenu, na kumwaga damu; je, mtaimiliki nchi hii?
Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.
Kwani huyo mtu atakayekula mafuta ya mnyama, ambaye ni katika wanyama ambao watu husongeza sadaka kwa BWANA kwa moto, mtu huyo atakayekula mafuta hayo atakatiliwa mbali na watu wake.
Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.
yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama.
Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;