Walawi 7:17 - Swahili Revised Union Version lakini hicho kitakachosalia, katika hizo nyama za sadaka, hata siku ya tatu kitachomwa moto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini nyama yoyote ya sadaka hiyo inayobaki hadi siku ya tatu itateketezwa. Biblia Habari Njema - BHND Lakini nyama yoyote ya sadaka hiyo inayobaki hadi siku ya tatu itateketezwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini nyama yoyote ya sadaka hiyo inayobaki hadi siku ya tatu itateketezwa. Neno: Bibilia Takatifu Nyama yoyote ya sadaka inayobaki hadi siku ya tatu lazima iteketezwe kwa moto. Neno: Maandiko Matakatifu Nyama yoyote ya sadaka inayobaki mpaka siku ya tatu lazima iteketezwe kwa moto. BIBLIA KISWAHILI lakini hicho kitakachosalia, katika hizo nyama za sadaka, hata siku ya tatu kitachomwa moto. |
Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.
wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote.
Lakini nyama yake huyo ng'ombe, na ngozi yake, na mavi yake, utayachoma kwa moto nje ya kambi; ni sadaka kwa ajili ya dhambi.
Na kwamba kitu chochote cha ile nyama, iliyo kwa ajili ya kuweka kwa kazi takatifu, au chochote cha hiyo mikate, kikisalia hata asubuhi, ndipo utavichoma kwa moto hivyo vilivyosalia; havitaliwa, maana, ni vitu vitakatifu.
Kisha Musa akamtafuta sana huyo mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye, tazama, alikuwa amekwisha kuteketezwa; naye akawakasirikia hao Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni, hao waliobaki, akawaambia,
Italiwa siku iyo hiyo mliyoichinja, na siku ya pili yake; na kama kitu chochote katika sadaka hiyo kilisalia hata siku ya tatu kitachomwa moto.