Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Walawi 6:13 - Swahili Revised Union Version

Moto utatunzwa uwake juu ya madhabahu daima; usizimike.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Moto utaendelea kuwaka daima juu ya madhabahu bila kuzimishwa kamwe.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Moto utaendelea kuwaka daima juu ya madhabahu bila kuzimishwa kamwe.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Moto utaendelea kuwaka daima juu ya madhabahu bila kuzimishwa kamwe.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Moto lazima uendelee kuwaka juu ya madhabahu mfululizo, kamwe usizimike.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Moto lazima uendelee kuwaka juu ya madhabahu mfululizo, kamwe usizimike.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Moto utatunzwa uwake juu ya madhabahu daima; usizimike.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Walawi 6:13
9 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe uwafanyie jambo hili, ili kuwaweka wakfu, wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani; twaa njeku mmoja, na kondoo dume wawili wasio na dosari,


na mkate usiotiwa chachu, na maandazi yasiyotiwa chachu yaliyokandwa kwa mafuta, na kaki zisizotiwa chachu zilizotiwa mafuta; utazifanya za unga mzuri mwembamba wa ngano.


tena, pamoja na mwana-kondoo mmoja utatoa vibaba vitatu vya unga mzuri uliochanganyika na mafuta yaliyopondwa, kiasi cha kibaba na robo kibaba; na divai kiasi cha kibaba na robo kibaba, iwe sadaka ya kinywaji.


Na mwamba wake utatoweka kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema BWANA, ambaye moto wake u katika Sayuni, na tanuri yake katika Yerusalemu.


Nacho chumba kinachokabili upande wa kaskazini ni cha makuhani, wasimamizi wa madhabahu; hao ni wana wa Sadoki, ambao kati ya wana wa Lawi, ndio waliomkaribia BWANA, ili kumtumikia.


Na huo moto ulio madhabahuni atautunza uwake daima juu yake, usizimike; naye kuhani atateketeza kuni katika moto huo kila siku asubuhi; naye ataipanga sadaka ya kuteketezwa juu yake, naye atayateketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake.


Na amri ya hiyo sadaka ya unga ni hii; wana wa Haruni wataisongeza mbele za BWANA, mbele ya madhabahu.


Haya, mwagize Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya sadaka ya kuteketezwa ni hii; hiyo sadaka ya kuteketezwa itakuwa pale motoni juu ya madhabahu usiku wote hadi asubuhi; na huo moto wa madhabahu utawaka juu yake usizimike.


Kisha moto ukatoka hapo mbele za BWANA, na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na yale mafuta juu ya madhabahu; watu wote walipouona huo moto wakapiga kelele wakainama kifudifudi.