na kuhani atamkadiria, akiwa mwema akiwa mbaya; kama kuhani atakavyomkadiria, ndivyo itakavyokuwa.
Walawi 27:23 - Swahili Revised Union Version ndipo kuhani atamhesabia kima cha kuhesabu kwako hata mwaka wa jubilii: naye atatoa siku hiyo kama hesabu yako, kuwa ni kitu kitakatifu kwa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kuhani ataamua thamani ya shamba hilo kwa kulingana na miaka iliyobaki kufikia mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini na mtu huyo atalazimika kulipa thamani yake kama ni kitu kitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND kuhani ataamua thamani ya shamba hilo kwa kulingana na miaka iliyobaki kufikia mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini na mtu huyo atalazimika kulipa thamani yake kama ni kitu kitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kuhani ataamua thamani ya shamba hilo kwa kulingana na miaka iliyobaki kufikia mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini na mtu huyo atalazimika kulipa thamani yake kama ni kitu kitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu lazima alipe thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu atalazimika kulipa thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwa bwana. BIBLIA KISWAHILI ndipo kuhani atamhesabia kima cha kuhesabu kwako hata mwaka wa jubilii: naye atatoa siku hiyo kama hesabu yako, kuwa ni kitu kitakatifu kwa BWANA. |
na kuhani atamkadiria, akiwa mwema akiwa mbaya; kama kuhani atakavyomkadiria, ndivyo itakavyokuwa.
Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya jubilii, ndipo kuhani atamhesabia hiyo fedha kama hesabu ya miaka iliyobaki hata mwaka wa jubilii, na kuhesabiwa kwako kutapunguzwa.
Tena kama akiweka wakfu kwa BWANA shamba ambalo amelinunua, ambalo si shamba la milki yake;
Mwaka wa jubilii shamba hilo litarejea kwake huyo ambaye lilinunuliwa kwake, yaani, huyo ambaye nchi hiyo ni milki yake.