ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki yake.
Walawi 27:18 - Swahili Revised Union Version Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya jubilii, ndipo kuhani atamhesabia hiyo fedha kama hesabu ya miaka iliyobaki hata mwaka wa jubilii, na kuhesabiwa kwako kutapunguzwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini kama akiliweka wakfu baada ya mwaka huo, basi, kuhani ataamua thamani yake kulingana na miaka iliyobaki kufikia mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini na thamani yake ipunguzwe. Biblia Habari Njema - BHND Lakini kama akiliweka wakfu baada ya mwaka huo, basi, kuhani ataamua thamani yake kulingana na miaka iliyobaki kufikia mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini na thamani yake ipunguzwe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini kama akiliweka wakfu baada ya mwaka huo, basi, kuhani ataamua thamani yake kulingana na miaka iliyobaki kufikia mwaka wa ukumbusho wa miaka hamsini na thamani yake ipunguzwe. Neno: Bibilia Takatifu Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya Yubile, kuhani ataweka thamani kulingana na idadi ya miaka iliyobaki kufikia Mwaka wa Yubile unaofuata, na thamani yake iliyoamuliwa itapunguzwa. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini kama akiweka shamba lake wakfu baada ya Yubile, kuhani ataweka thamani kulingana na idadi ya miaka iliyobaki kufikia Mwaka wa Yubile unaofuata, na thamani yake iliyoamuliwa itapunguzwa. BIBLIA KISWAHILI Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya jubilii, ndipo kuhani atamhesabia hiyo fedha kama hesabu ya miaka iliyobaki hata mwaka wa jubilii, na kuhesabiwa kwako kutapunguzwa. |
ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki yake.
Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa BWANA ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa.
Ikiwa anaweka shamba lake liwe wakfu tangu mwaka wa jubilii, litakadiriwa vivyo hivyo kama hesabu yako ilivyo.
Na kama yeye aliyeliweka shamba wakfu akitaka kulikomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nalo litathibitishwa kwake.
ndipo kuhani atamhesabia kima cha kuhesabu kwako hata mwaka wa jubilii: naye atatoa siku hiyo kama hesabu yako, kuwa ni kitu kitakatifu kwa BWANA.