Yeye hatamgeuza, wala kumbadili mwema kwa mbaya, au mbaya kwa mwema; ikiwa atabadili mnyama kwa mnyama yeyote, ndipo mnyama huyo na yule waliobadiliwa wote wawili watakuwa watakatifu.
Walawi 27:11 - Swahili Revised Union Version Na kama ni mnyama yeyote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa BWANA, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kama nadhiri hiyo yahusu mnyama najisi, wa aina ambayo si halali kumtolea Mwenyezi-Mungu, basi, mtu aliyemtoa, atamleta kwa kuhani, Biblia Habari Njema - BHND “Kama nadhiri hiyo yahusu mnyama najisi, wa aina ambayo si halali kumtolea Mwenyezi-Mungu, basi, mtu aliyemtoa, atamleta kwa kuhani, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kama nadhiri hiyo yahusu mnyama najisi, wa aina ambayo si halali kumtolea Mwenyezi-Mungu, basi, mtu aliyemtoa, atamleta kwa kuhani, Neno: Bibilia Takatifu Kama alichokiwekea nadhiri ni mnyama aliye najisi, yaani yule asiyekubalika kuwa sadaka kwa Mwenyezi Mungu, huyo mnyama lazima aletwe kwa kuhani, Neno: Maandiko Matakatifu Kama alichokiwekea nadhiri ni mnyama aliye najisi kiibada, yaani yule asiye kubalika kuwa sadaka kwa bwana, huyo mnyama lazima aletwe kwa kuhani, BIBLIA KISWAHILI Na kama ni mnyama yeyote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa BWANA, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani; |
Yeye hatamgeuza, wala kumbadili mwema kwa mbaya, au mbaya kwa mwema; ikiwa atabadili mnyama kwa mnyama yeyote, ndipo mnyama huyo na yule waliobadiliwa wote wawili watakuwa watakatifu.
na kuhani atamkadiria, akiwa mwema akiwa mbaya; kama kuhani atakavyomkadiria, ndivyo itakavyokuwa.
Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.
Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yoyote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili.