Na kundi kubwa la watu waliochangamana mno wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng'ombe, wanyama wengi sana.
Walawi 24:10 - Swahili Revised Union Version Ikawa mwanamume mmoja ambaye mama yake ni Mwisraeli, na babaye ni Mmisri, alitokea kati ya wana wa Israeli akalikufuru; na kupigana na Mwisraeli katika kambi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku moja kukatokea mzozo huko kambini kati ya Mwisraeli mmoja na kijana mmoja wa mama Mwisraeli aitwaye Shelomithi lakini baba Mmisri. Biblia Habari Njema - BHND Siku moja kukatokea mzozo huko kambini kati ya Mwisraeli mmoja na kijana mmoja wa mama Mwisraeli aitwaye Shelomithi lakini baba Mmisri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku moja kukatokea mzozo huko kambini kati ya Mwisraeli mmoja na kijana mmoja wa mama Mwisraeli aitwaye Shelomithi lakini baba Mmisri. Neno: Bibilia Takatifu Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alienda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli. Neno: Maandiko Matakatifu Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli. BIBLIA KISWAHILI Ikawa mwanamume mmoja ambaye mama yake ni Mwisraeli, na babaye ni Mmisri, alitokea kati ya wana wa Israeli akalikufuru; na kupigana na Mwisraeli katika kambi; |
Na kundi kubwa la watu waliochangamana mno wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng'ombe, wanyama wengi sana.
kisha huyo mwanamume ambaye mama ni Mwisraeli akakufuru jina la Bwana na kulaani nao watu wakampeleka kwa Musa. Mama yake mtu huyo alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila la Dani.
Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zitolewazo kwa BWANA kwa moto, kwa amri ya milele.
Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, Ni nani atakayetupa nyama tule?