Mtu yeyote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu yeyote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atatengwa mbali na watu wake.
Walawi 19:8 - Swahili Revised Union Version lakini kila mtu atakayekula atalipizwa uovu wake mwenyewe, kwa sababu amekinajisi kitu hicho kitakatifu cha BWANA; na mtu huyo atatengwa na watu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema naye atakayekula nyama hiyo ni lazima awajibike kwa uovu wake kwa sababu amekitia unajisi kitu kitakatifu cha Mwenyezi-Mungu. Mtu huyo atatengwa na watu wake. Biblia Habari Njema - BHND naye atakayekula nyama hiyo ni lazima awajibike kwa uovu wake kwa sababu amekitia unajisi kitu kitakatifu cha Mwenyezi-Mungu. Mtu huyo atatengwa na watu wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza naye atakayekula nyama hiyo ni lazima awajibike kwa uovu wake kwa sababu amekitia unajisi kitu kitakatifu cha Mwenyezi-Mungu. Mtu huyo atatengwa na watu wake. Neno: Bibilia Takatifu Yeyote atakayekula atawajibishwa, kwa sababu amenajisi kitu kilicho kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu; mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake. Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote atakayekula atawajibishwa, kwa sababu amenajisi kitu kilicho kitakatifu kwa bwana; mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake. BIBLIA KISWAHILI lakini kila mtu atakayekula atalipizwa uovu wake mwenyewe, kwa sababu amekinajisi kitu hicho kitakatifu cha BWANA; na mtu huyo atatengwa na watu wake. |
Mtu yeyote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu yeyote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atatengwa mbali na watu wake.
Na mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa katika pembe za shamba lako, wala usiyakusanye masazo ya mavuno yako;
Na mtu yeyote akifanya dhambi, kwa kuwa ameisikia sauti yenye kuapisha, naye akawa ni shahidi, kwamba aliona au kujua, asipolifunua neno lile, ndipo atakapochukua uovu wake mwenyewe;
lakini mtu huyo atakayekula katika nyama ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, na unajisi wake akiwa nao juu yake, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.
Kisha mtu awaye yote atakapogusa kitu chochote kilicho najisi, uchafu wa binadamu, au mnyama aliye najisi, au machukizo yoyote yaliyo najisi, kisha akala nyama ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.