Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;
Walawi 15:11 - Swahili Revised Union Version Na mtu yeyote atakayeguswa na mwenye kisonono, ambaye hajanawa mikono yake majini, atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu yeyote anayetokwa na usaha akimgusa mtu bila kusafisha kwanza mikono yake na kuoga, aliyeguswa atakuwa najisi mpaka jioni. Biblia Habari Njema - BHND Mtu yeyote anayetokwa na usaha akimgusa mtu bila kusafisha kwanza mikono yake na kuoga, aliyeguswa atakuwa najisi mpaka jioni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu yeyote anayetokwa na usaha akimgusa mtu bila kusafisha kwanza mikono yake na kuoga, aliyeguswa atakuwa najisi mpaka jioni. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Yeyote atakayeguswa na mtu anayetokwa na usaha bila kunawa mikono yake kwa maji, ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Yeyote atakayeguswa na mtu anayetokwa na usaha bila kunawa mikono yake kwa maji, ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi mpaka jioni. BIBLIA KISWAHILI Na mtu yeyote atakayeguswa na mwenye kisonono, ambaye hajanawa mikono yake majini, atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. |
Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;
Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote kilichokuwa chini yake huyo atakuwa najisi hadi jioni; na mtu atakayevichukua vitu vile atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
Na chombo cha udongo ambacho amekigusa mwenye kisonono, kitavunjwavunjwa; na kila chombo cha mti kitaoshwa majini.
Na kitu chochote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hadi jioni.
lakini na iwe ikaribiapo jioni, yeye ataoga maji; na jua likiisha kuchwa ataingia ndani ya kituo.