Na kama kuhani akitazama, ikiwa hilo pigo halikuenea katika hilo vazi, wala katika hilo lililofumwa, wala katika hilo lililosokotwa, wala katika kitu chochote cha ngozi;
Walawi 13:54 - Swahili Revised Union Version ndipo kuhani ataamuru kwamba wakifue kitu kile kilicho na hilo pigo, naye atakiweka mahali muda wa siku saba tena; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ataamuru vazi hilo lifuliwe na kuwekwa kando kwa muda mwingine wa siku saba. Biblia Habari Njema - BHND ataamuru vazi hilo lifuliwe na kuwekwa kando kwa muda mwingine wa siku saba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ataamuru vazi hilo lifuliwe na kuwekwa kando kwa muda mwingine wa siku saba. Neno: Bibilia Takatifu ataagiza kwamba vazi lenye maambukizo lisafishwe. Kisha atalitenga kwa siku nyingine saba. Neno: Maandiko Matakatifu ataagiza kwamba kifaa chenye maambukizo kisafishwe. Kisha atakitenga kwa siku saba. BIBLIA KISWAHILI ndipo kuhani ataamuru kwamba wakifue kitu kile kilicho na hilo pigo, naye atakiweka mahali muda wa siku saba tena; |
Na kama kuhani akitazama, ikiwa hilo pigo halikuenea katika hilo vazi, wala katika hilo lililofumwa, wala katika hilo lililosokotwa, wala katika kitu chochote cha ngozi;
kisha kuhani ataangalia, baada ya kuoshwa hilo pigo; ikiwa hilo pigo halikugeuka rangi yake, wala halikuenea, ni najisi; utaliteketeza; ni uharibifu likiwa lina doa ndani au nje.