na mahali palipokuwa na lile jipu pana uvimbe mweupe, au kipaku king'aacho, cheupe lakini chekundu kidogo, ndipo atamwonesha kuhani mahali hapo;
Walawi 13:42 - Swahili Revised Union Version Lakini kwamba katika kile kichwa kilicho na upara, au kile kipaji kilicho na upara, laonekana pigo jeupe kisha jekundu kidogo; ni ukoma, unatokea katika kichwa chake cha upara, au katika kipaji chake cha upara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini kama kwenye kichwa penye upara au kwenye paji la uso penye upara kuna alama nyekundu-nyeupe, huo ni ukoma unaotokea kwenye upara wake kichwani au kwenye paji lake. Biblia Habari Njema - BHND Lakini kama kwenye kichwa penye upara au kwenye paji la uso penye upara kuna alama nyekundu-nyeupe, huo ni ukoma unaotokea kwenye upara wake kichwani au kwenye paji lake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini kama kwenye kichwa penye upara au kwenye paji la uso penye upara kuna alama nyekundu-nyeupe, huo ni ukoma unaotokea kwenye upara wake kichwani au kwenye paji lake. Neno: Bibilia Takatifu Lakini kama ana kidonda chenye wekundu na weupe kwenye kichwa chake chenye upara, au kwenye paji la uso, ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza unaojitokeza kichwani au kwenye paji lake la uso. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini kama ana kidonda chenye wekundu na weupe kwenye kichwa chake chenye upaa, au kwenye paji la uso, ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza unaojitokeza kichwani au kwenye paji lake la uso. BIBLIA KISWAHILI Lakini kwamba katika kile kichwa kilicho na upara, au kile kipaji kilicho na upara, laonekana pigo jeupe kisha jekundu kidogo; ni ukoma, unatokea katika kichwa chake cha upara, au katika kipaji chake cha upara. |
na mahali palipokuwa na lile jipu pana uvimbe mweupe, au kipaku king'aacho, cheupe lakini chekundu kidogo, ndipo atamwonesha kuhani mahali hapo;
Mtu atakapokuwa na uvimbe katika ngozi ya mwili wake, au upele, au kipaku king'aacho, nao ukawa ni ugonjwa wa ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa mmojawapo wa wanawe makuhani;
Tena kwamba nywele za mtu zimemtoka kichwani upande wa mbele, yeye ni mwenye upara wa kipaji; ni safi.
Ndipo kuhani atamwangalia; kivimbe cha pigo kikiwa cheupe na chekundu chekundu, katika kichwa chake chenye upara, au katika kipaji chake cha upara, kama vile kuonekana kwa ukoma katika ngozi ya mwili;
naye ataliangalia hilo pigo, na tazama, likiwa pigo limo ndani ya kuta za nyumba, nalo lina mashimo-mashimo, rangi ya majani, au mekundu, na kuonekana kuingia ndani kuliko huo ukuta;