ndipo kuhani ataliangalia hilo pigo; ikiwa pigo limeingia ndani kuliko ngozi yenyewe, na nywele zilizomo kuwa za rangi ya manjano na nyembamba, ndipo kuhani atasema kwamba ni najisi, maana ni kipwepwe, ni ukoma wa kichwa au wa kindevu.
Walawi 13:37 - Swahili Revised Union Version Lakini akiona ya kuwa hicho kipwepwe kimepungua, na nywele nyeusi zimemea humo; hicho kipwepwe kimepoa, naye yu safi, na huyo kuhani atasema kwamba yu safi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini iwapo kuhani ataona kuwa vile vipele vimepona na nywele nyeusi zimeota mahali hapo, basi, vidonda hivyo vimepona, basi, mtu huyo ni safi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi. Biblia Habari Njema - BHND Lakini iwapo kuhani ataona kuwa vile vipele vimepona na nywele nyeusi zimeota mahali hapo, basi, vidonda hivyo vimepona, basi, mtu huyo ni safi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini iwapo kuhani ataona kuwa vile vipele vimepona na nywele nyeusi zimeota mahali hapo, basi, vidonda hivyo vimepona, basi, mtu huyo ni safi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi. Neno: Bibilia Takatifu Hata hivyo, katika uchunguzi wake akiona hapajabadilika, na nywele nyeusi zimeota juu yake, huyo mtu amepona. Yeye si najisi; kuhani atamtangaza kuwa safi. Neno: Maandiko Matakatifu Hata hivyo, katika uchunguzi wake akiona hapajabadilika, na nywele nyeusi zimeota juu yake, upele umepona. Yeye si najisi, kuhani atamtangaza kuwa safi. BIBLIA KISWAHILI Lakini akiona ya kuwa hicho kipwepwe kimepungua, na nywele nyeusi zimemea humo; hicho kipwepwe kimepoa, naye yu safi, na huyo kuhani atasema kwamba yu safi. |
ndipo kuhani ataliangalia hilo pigo; ikiwa pigo limeingia ndani kuliko ngozi yenyewe, na nywele zilizomo kuwa za rangi ya manjano na nyembamba, ndipo kuhani atasema kwamba ni najisi, maana ni kipwepwe, ni ukoma wa kichwa au wa kindevu.
ndipo kuhani atamwangalia; na ikiwa hicho kipwepwe kimeenea katika ngozi yake, kuhani hatatafuta hizo nywele za rangi ya manjano; yeye ni najisi.
Mwanamume au mwanamke, atakapokuwa na vipaku ving'aavyo katika ngozi ya mwili, vipaku ving'aavyo vyeupe;