Wafilipi 4:4 - Swahili Revised Union Version Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini! Biblia Habari Njema - BHND Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: furahini! Neno: Bibilia Takatifu Furahini katika Bwana Isa siku zote, tena nasema furahini! Neno: Maandiko Matakatifu Furahini katika Bwana Isa siku zote, tena nasema furahini! BIBLIA KISWAHILI Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema, Furahini. |
Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Lakini ilipokuwa karibu usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo.
kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria, na alaaniwe.
Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi.
Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili pia katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.