Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.
Wafilipi 4:16 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilipokuwa nahitaji msaada kule Thesalonike mliniletea, tena zaidi ya mara moja. Biblia Habari Njema - BHND Nilipokuwa nahitaji msaada kule Thesalonike mliniletea, tena zaidi ya mara moja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilipokuwa nahitaji msaada kule Thesalonike mliniletea, tena zaidi ya mara moja. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana hata nilipokuwa huko Thesalonike, mliniletea msaada kwa ajili ya mahitaji yangu zaidi ya mara moja. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana hata nilipokuwa huko Thesalonike, mliniletea msaada kwa ajili ya mahitaji yangu zaidi ya mara moja. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. |
Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.
Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, nilitaka kuja mara kwa mara, lakini Shetani akatuzuia.
Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, huku tukiwahubiria Injili ya Mungu.
Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.