Nami nitakuvutia Sisera, kamanda wa jeshi la Yabini, hadi mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako.
Waamuzi 4:8 - Swahili Revised Union Version Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baraki akamwambia Debora, “Kama utakwenda pamoja nami, nitakwenda. Lakini usipokwenda pamoja nami, sitakwenda.” Biblia Habari Njema - BHND Baraki akamwambia Debora, “Kama utakwenda pamoja nami, nitakwenda. Lakini usipokwenda pamoja nami, sitakwenda.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baraki akamwambia Debora, “Kama utakwenda pamoja nami, nitakwenda. Lakini usipokwenda pamoja nami, sitakwenda.” Neno: Bibilia Takatifu Baraka akamwambia, “Ukienda pamoja nami nitaenda, lakini usipoenda pamoja nami, sitaenda.” Neno: Maandiko Matakatifu Baraka akamwambia, “Ukienda pamoja nami nitakwenda, lakini usipokwenda pamoja nami, sitakwenda.” BIBLIA KISWAHILI Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi. |
Nami nitakuvutia Sisera, kamanda wa jeshi la Yabini, hadi mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako.
Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana BWANA atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi.