Kwa hiyo akawaambia watumishi wake, Tazameni, shamba la Yoabu liko karibu na shamba langu, naye ana shayiri huko; nendeni mkalitie moto. Basi watumishi wa Absalomu wakalitia moto lile shamba.
Waamuzi 15:3 - Swahili Revised Union Version Samsoni akasema, Safari hii nitakuwa sina hatia kwa hawa Wafilisti, hapo nitakapowadhuru. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Samsoni akamwambia, “Safari hii sitakuwa na lawama kwa yale nitakayowatendea Wafilisti.” Biblia Habari Njema - BHND Samsoni akamwambia, “Safari hii sitakuwa na lawama kwa yale nitakayowatendea Wafilisti.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Samsoni akamwambia, “Safari hii sitakuwa na lawama kwa yale nitakayowatendea Wafilisti.” Neno: Bibilia Takatifu Samsoni akawaambia, “Wakati huu, nitakapowadhuru Wafilisti, sitakuwa na lawama.” Neno: Maandiko Matakatifu Samsoni akawaambia, “Wakati huu, nitakapowadhuru Wafilisti, sitakuwa na lawama.” BIBLIA KISWAHILI Samsoni akasema, Safari hii nitakuwa sina hatia kwa hawa Wafilisti, hapo nitakapowadhuru. |
Kwa hiyo akawaambia watumishi wake, Tazameni, shamba la Yoabu liko karibu na shamba langu, naye ana shayiri huko; nendeni mkalitie moto. Basi watumishi wa Absalomu wakalitia moto lile shamba.
Ikawa kwa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, Mbembeleze mumeo, ili atutegulie hicho kitendawili, tusije tukakuteketeza moto wewe na nyumba ya baba yako; je! Mmetuita ili mpate kuichukua mali yetu? Je! Sivyo?
Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la BWANA; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli.
Baba yake akasema, Hakika mimi nilidhani ya kuwa umemchukia kabisa; basi nilimpa rafiki yako. Je! Si dada yake mdogo ni mzuri kuliko yeye? Tafadhali, mtwae huyo badala yake.
Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu; kisha akatwaa mienge ya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia mwenge kati ya kila mikia miwili.