Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, BWANA, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.
Ufunuo 22:13 - Swahili Revised Union Version Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.” Biblia Habari Njema - BHND Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.” Neno: Bibilia Takatifu Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho. Neno: Maandiko Matakatifu Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho. BIBLIA KISWAHILI Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. |
Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, BWANA, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.
BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.
Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia.
ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika kitabu, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.
Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye aliye na kiu, maji kutoka chemchemi ya maji ya uzima, bure.
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.