Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Ufunuo 21:9 - Swahili Revised Union Version

Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba yaliyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana-kondoo.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba yaliyokuwa yamejaa mabaa saba ya mwisho, akaja na kuniambia, “Njoo! Nami nitakuonesha bibi arusi, mkewe Mwanakondoo!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba yaliyokuwa yamejaa mabaa saba ya mwisho, akaja na kuniambia, “Njoo! Nami nitakuonesha bibi arusi, mkewe Mwanakondoo!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba yaliyokuwa yamejaa mabaa saba ya mwisho, akaja na kuniambia, “Njoo! Nami nitakuonesha bibi arusi, mkewe Mwanakondoo!”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba ya hayo mapigo saba ya mwisho akaja akaniambia, “Njoo, nami nitakuonesha bibi arusi, yaani mke wa Mwana-Kondoo.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba ya hayo mapigo saba ya mwisho akaja akaniambia, “Njoo, nami nitakuonyesha bibi arusi, yaani, mke wa Mwana-Kondoo.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba yaliyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonesha yule Bibi harusi, mke wa Mwana-kondoo.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Ufunuo 21:9
10 Marejeleo ya Msalaba  

Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaoneshe watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonesha mtumwa wake Yohana;


Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye yale mabakuli saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;


Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.


Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia moja na arubaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, ambacho malaika alitumia.


Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.


Kisha akanionesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-kondoo,


Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.


Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.