Akaupima urefu wake; dhiraa ishirini, na upana wake, dhiraa ishirini, mbele ya hekalu; akaniambia, Hapa ndipo mahali patakatifu kuliko kila mahali.
Ufunuo 21:16 - Swahili Revised Union Version Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake ni sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu moja na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: Ulikuwa na urefu, upana na kimo cha kama kilomita 2,400. Biblia Habari Njema - BHND Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: Ulikuwa na urefu, upana na kimo cha kama kilomita 2,400. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mji wenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa. Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: ulikuwa na urefu, upana na kimo cha kama kilomita 2,400. Neno: Bibilia Takatifu Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama stadioni 12,000; urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa. Neno: Maandiko Matakatifu Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama kilomita 2,200; urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa. BIBLIA KISWAHILI Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake ni sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu moja na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. |
Akaupima urefu wake; dhiraa ishirini, na upana wake, dhiraa ishirini, mbele ya hekalu; akaniambia, Hapa ndipo mahali patakatifu kuliko kila mahali.
Alipima pande zake zote nne; lilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mianzi mia tano, ili kupatenga mahali palipo patakatifu, na mahali ambapo ni pa watu wote.
Kuuzunguka ni mianzi elfu kumi na nane; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo.
Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.
Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia moja na arubaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, ambacho malaika alitumia.