Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.
Tito 3:10 - Swahili Revised Union Version Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, tengana naye; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu anayesababisha mafarakano mpe onyo la kwanza na la pili, kisha achana naye. Biblia Habari Njema - BHND Mtu anayesababisha mafarakano mpe onyo la kwanza na la pili, kisha achana naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu anayesababisha mafarakano mpe onyo la kwanza na la pili, kisha achana naye. Neno: Bibilia Takatifu Mtu anayesababisha mafarakano, mwonye mara ya kwanza, kisha mwonye mara ya pili. Baada ya hapo, usihusike naye tena. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu anayesababisha mafarakano, mwonye mara ya kwanza, kisha mwonye mara ya pili. Baada ya hapo, usihusike naye tena. BIBLIA KISWAHILI Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, tengana naye; |
Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.
Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia;
Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la barua hii, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari;
Ndugu, tunawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu kutoka kwa kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.
Lakini kulitokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.