Tito 2:6 - Swahili Revised Union Version Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi. Biblia Habari Njema - BHND Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kadhalika, wahimize vijana wawe na kiasi. Neno: Bibilia Takatifu Vivyo hivyo, himiza vijana wawe na kiasi. Neno: Maandiko Matakatifu Vivyo hivyo, himiza vijana wawe na kiasi. BIBLIA KISWAHILI Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; |
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, wa kiume na wa kike, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba.