Na katika Walawi; Ahia mtunzaji wa hazina ya nyumba ya Mungu, pamoja na hazina ya vitu vilivyowekwa wakfu.
Nehemia 11:16 - Swahili Revised Union Version na Shabethai na Yozabadi, wa wakuu wa Walawi, walioisimamia kazi ya nje ya nyumba ya Mungu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shabethai na Yozabadi, wakuu wa ukoo wa Walawi, walikuwa wasimamizi wa kazi za nje ya nyumba ya Mungu, Biblia Habari Njema - BHND Shabethai na Yozabadi, wakuu wa ukoo wa Walawi, walikuwa wasimamizi wa kazi za nje ya nyumba ya Mungu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shabethai na Yozabadi, wakuu wa ukoo wa Walawi, walikuwa wasimamizi wa kazi za nje ya nyumba ya Mungu, Neno: Bibilia Takatifu Shabethai na Yozabadi, viongozi wawili wa Walawi, ambao walisimamia kazi za nje za nyumba ya Mungu; Neno: Maandiko Matakatifu Shabethai na Yozabadi, viongozi wawili wa Walawi, ambao walisimamia kazi za nje za nyumba ya Mungu; BIBLIA KISWAHILI na Shabethai na Yozabadi, wa wakuu wa Walawi, walioisimamia kazi ya nje ya nyumba ya Mungu; |
Na katika Walawi; Ahia mtunzaji wa hazina ya nyumba ya Mungu, pamoja na hazina ya vitu vilivyowekwa wakfu.
Katika Waishari, Kenania na wanawe walikuwa kwa ajili ya kazi ya nje juu ya Israeli, kuwa maofisa na waamuzi.
Yonathani, mwana wa Asaheli, na Yazeya, mwana wa Tikwa, hawa peke yao ndio waliosimama kulipinga neno hilo; na Meshulamu, na Shabethai Mlawi, wakawasaidia.
Hata siku ya nne, hizo fedha na dhahabu na vile vyombo vilipimwa ndani ya nyumba ya Mungu, vikatiwa mikononi mwa Meremothi, mwana wa Uria, kuhani; na pamoja naye alikuwapo Eleazari, mwana wa Finehasi; na pamoja nao Yozabadi, mwana wa Yeshua, na Noadia, mwana wa Binui, Walawi;
Na wa Walawi; Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni;
na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu, mkuu wa kuanzisha shukrani katika sala, na Bakbukia, wa pili wake miongoni mwa nduguze; na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.
Tena Yeshua, na Bani, na Sherebia, na Yamini, na Akubu, na Shabethai, na Hodai, na Maaseya, na Kelita, na Azaria, na Yozabadi, na Hanani, na Pelaya, nao ni Walawi, wakawafahamisha watu torati; na watu wakasimama mahali pao.