Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Nehemia 10:33 - Swahili Revised Union Version

kwa mikate mitakatifu, na kwa sadaka ya unga ya daima, na kwa sadaka ya kuteketezwa ya daima, ya sabato, na ya siku za mwezi mpya, na ya sikukuu, tena kwa vitu vile vitakatifu, na kwa sadaka za dhambi, za kuwafanyia Israeli upatanisho, na kwa ajili ya kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mikate mitakatifu, sadaka za nafaka za kawaida, sadaka za kuteketezwa za kawaida, sadaka za siku za Sabato, sikukuu za mwandamo wa mwezi, sikukuu nyingine zilizowekwa, vitu vingine vitakatifu, sadaka za kuondoa dhambi, ili kuwafanyia upatanisho watu wa Israeli na kazi nyingine zozote za nyumba ya Mungu wetu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

mikate mitakatifu, sadaka za nafaka za kawaida, sadaka za kuteketezwa za kawaida, sadaka za siku za Sabato, sikukuu za mwandamo wa mwezi, sikukuu nyingine zilizowekwa, vitu vingine vitakatifu, sadaka za kuondoa dhambi, ili kuwafanyia upatanisho watu wa Israeli na kazi nyingine zozote za nyumba ya Mungu wetu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa ajili ya mikate ya Wonesho, kwa ajili ya sadaka za kawaida za nafaka na sadaka za kuteketezwa, kwa ajili ya sadaka za siku za Sabato, Sikukuu za Mwandamo wa Mwezi na sikukuu nyingine zilizoamriwa, kwa ajili ya sadaka takatifu, kwa ajili ya sadaka za dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, na kwa ajili ya kazi zote za nyumba ya Mungu wetu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa ajili ya mikate ya Wonyesho, kwa ajili ya sadaka za kawaida za nafaka na sadaka za kuteketezwa, kwa ajili ya sadaka za siku za Sabato, Sikukuu za Mwandamo wa Mwezi na sikukuu nyingine zilizoamriwa, kwa ajili ya sadaka takatifu, kwa ajili ya sadaka za dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, na kwa ajili ya kazi zote za nyumba ya Mungu wetu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

kwa mikate mitakatifu, na kwa sadaka ya unga ya daima, na kwa sadaka ya kuteketezwa ya daima, ya sabato, na ya siku za mwezi mpya, na ya sikukuu, tena kwa vitu vile vitakatifu, na kwa sadaka za dhambi, za kuwafanyia Israeli upatanisho, na kwa ajili ya kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Nehemia 10:33
7 Marejeleo ya Msalaba  

Angalia, najenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wangu, ili kumfanyia wakfu, ya kufukizia mbele zake fukizo la manukato, na ya mkate wa wonyesho wa daima, na ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na za siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa za BWANA, Mungu wetu. Hili ni agizo la milele kwa Israeli.

Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.