Nahumu 1:13 - Swahili Revised Union Version Na sasa nitakuvunjia nira yake, nami nitayakata mafungo yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa nitaivunja nira ya Ashuru shingoni mwenu, na minyororo waliyowafungia nitaikatakata.” Biblia Habari Njema - BHND Sasa nitaivunja nira ya Ashuru shingoni mwenu, na minyororo waliyowafungia nitaikatakata.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa nitaivunja nira ya Ashuru shingoni mwenu, na minyororo waliyowafungia nitaikatakata.” Neno: Bibilia Takatifu Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako, nami nitazivunjilia mbali pingu zako.” Neno: Maandiko Matakatifu Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako, nami nitazivunjilia mbali pingu zako.” BIBLIA KISWAHILI Na sasa nitakuvunjia nira yake, nami nitayakata mafungo yako. |
Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.
kwamba nitamvunja huyo Mwashuri vipande vipande katika nchi yangu, na juu ya mlima wangu nitamkanyaga chini ya miguu yangu; ndipo nira yake iliyo juu yao itakapoondoka, na mzigo wake utatoka mabegani mwao.
Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani.
Kwa maana tangu zamani wewe umeivunja nira yako, na kuvipasua vifungo vyako; ukasema, Mimi sitatumika; kwa maana juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi, umejiinamisha, ukafanya mambo ya ukahaba.
nitawaendea watu wakubwa, nami nitasema nao; kwa maana hao wanaijua njia ya BWANA, na hukumu ya Mungu wao. Bali hawa kwa nia moja wameivunja nira, na kuvikata vifungo.
Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawafanya mwende sawasawa.