Akasema, Mwanangu hatashuka pamoja nanyi, maana nduguye amekufa, naye amesalia peke yake; mabaya yakimpata katika njia mtakayoiendea ndipo mtakaposhusha mvi zangu kwa sikitiko mpaka kaburini.
Mwanzo 43:13 - Swahili Revised Union Version Mtwaeni na ndugu yenu, mwondoke na kurudi kwa mtu yule. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mchukueni pia ndugu yenu mwende kwa huyo mtu. Biblia Habari Njema - BHND Mchukueni pia ndugu yenu mwende kwa huyo mtu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mchukueni pia ndugu yenu mwende kwa huyo mtu. Neno: Bibilia Takatifu Mchukueni ndugu yenu pia, mrudi kwa huyo mtu mara moja. Neno: Maandiko Matakatifu Mchukueni ndugu yenu pia mrudi kwa huyo mtu mara moja. BIBLIA KISWAHILI Mtwaeni na ndugu yenu, mwondoke na kurudi kwa mtu yule. |
Akasema, Mwanangu hatashuka pamoja nanyi, maana nduguye amekufa, naye amesalia peke yake; mabaya yakimpata katika njia mtakayoiendea ndipo mtakaposhusha mvi zangu kwa sikitiko mpaka kaburini.
Mkatwae fedha maradufu mikononi mwenu, na fedha zile zilizorudishwa kinywani mwa magunia yenu zirudisheni mikononi mwenu; labda zilisahauliwa.
Mungu Mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu huyo mwingine, na Benyamini. Nami nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa.