Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng'ombe, na punda dume, na watumwa, na wajakazi, na punda majike, na ngamia.
Mwanzo 20:14 - Swahili Revised Union Version Basi Abimeleki akatwaa kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi, akampa Abrahamu, akamrudishia Sara mkewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abimeleki akamrudishia Abrahamu mke wake Sara, akampa na kondoo, ng'ombe na watumwa wa kiume na kike. Biblia Habari Njema - BHND Abimeleki akamrudishia Abrahamu mke wake Sara, akampa na kondoo, ng'ombe na watumwa wa kiume na kike. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abimeleki akamrudishia Abrahamu mke wake Sara, akampa na kondoo, ng'ombe na watumwa wa kiume na kike. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Abimeleki akatwaa kondoo na ng’ombe, na watumwa wa kiume na wa kike, akampa Ibrahimu, na akamrudisha Sara kwa mumewe. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Abimeleki akatwaa kondoo na ng’ombe, na watumwa wa kiume na wa kike akampa Ibrahimu, akamrudisha Sara kwa mumewe. BIBLIA KISWAHILI Basi Abimeleki akatwaa kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi, akampa Abrahamu, akamrudishia Sara mkewe. |
Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng'ombe, na punda dume, na watumwa, na wajakazi, na punda majike, na ngamia.
Abrahamu akasema, Kwa kuwa niliona, hakika hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu.
Abrahamu akanena juu ya Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu”. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wakamtwaa Sara.
Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao.
Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Abrahamu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda.
Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga watumwa wenzake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;