Mwanzo 15:19 - Swahili Revised Union Version Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema yaani nchi za Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, Biblia Habari Njema - BHND yaani nchi za Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza yaani nchi za Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, Neno: Bibilia Takatifu yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, Neno: Maandiko Matakatifu yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, BIBLIA KISWAHILI Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni, |
nawe ukauona moyo wake kuwa mwaminifu mbele zako, ukafanya agano naye, kumpa nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Myebusi, na Mgirgashi, naam, kuwapa wazao wake; nawe umetimiza ahadi yako kwani u mwenye haki.
Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.
Nami nimesema, Nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misri na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, nchi ijaayo maziwa na asali.
nami nimeshuka ili niwaokoe kutoka kwa mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hadi nchi njema, kisha pana; nchi itiririkayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
Nanyi mliuvuka Yordani, mkafika Yeriko; nao watu wa Yeriko wakapigana nanyi, Mwamori, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhiti, na Mgirgashi, na Mhivi, na Myebusi; nami nikawatia mikononi mwenu.
Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Nendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki.