Maana tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
Mhubiri 9:4 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini anayeambatana na walio hai analo bado tumaini, afadhali mbwa hai kuliko simba mfu. Biblia Habari Njema - BHND Lakini anayeambatana na walio hai analo bado tumaini, afadhali mbwa hai kuliko simba mfu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini anayeambatana na walio hai analo bado tumaini, afadhali mbwa hai kuliko simba mfu. Neno: Bibilia Takatifu Yeyote aliye miongoni mwa walio hai analo tumaini, hata mbwa hai ni bora kuliko simba aliyekufa! Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote aliye miongoni mwa walio hai analo tumaini, hata mbwa hai ni bora kuliko simba aliyekufa! BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa; |
Maana tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu.
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana tuzo tena; maana hata kumbukumbu lao limesahauliwa.
Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuutumainia uaminifu wako.