Mhubiri 7:8 - Swahili Revised Union Version Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwisho wa jambo ni afadhali kuliko mwanzo wake; mvumilivu rohoni ni bora kuliko mwenye majivuno. Biblia Habari Njema - BHND Mwisho wa jambo ni afadhali kuliko mwanzo wake; mvumilivu rohoni ni bora kuliko mwenye majivuno. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwisho wa jambo ni afadhali kuliko mwanzo wake; mvumilivu rohoni ni bora kuliko mwenye majivuno. Neno: Bibilia Takatifu Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake, uvumilivu ni bora kuliko kiburi. Neno: Maandiko Matakatifu Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake, uvumilivu ni bora kuliko kiburi. BIBLIA KISWAHILI Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi. |
Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.
Abrahamu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo yako mema katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unateseka.
Angalieni, twawaita heri wao waliostahimili. Mmesikia habari za kustahimili kwake Ayubu, kuona mwisho Bwana aliyomtendea, jinsi Bwana alivyo mwingi wa rehema na mwenye huruma.
Kwa hiyo iweni tayari, na makini; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.