Methali 17:28 - Swahili Revised Union Version Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima; akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili. Biblia Habari Njema - BHND Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima; akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima; akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili. Neno: Bibilia Takatifu Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima akinyamaza, na mwenye ufahamu akiuzuia ulimi wake. Neno: Maandiko Matakatifu Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza, na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake. BIBLIA KISWAHILI Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu. |
Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni, Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena;
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.
Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza?
Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu.
Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.