Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.
Mathayo 7:20 - Swahili Revised Union Version Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao. BIBLIA KISWAHILI Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. |
Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.
Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.
Basi sasa nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa,
Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.