Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
Mathayo 7:19 - Swahili Revised Union Version Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni. Biblia Habari Njema - BHND Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni. Neno: Bibilia Takatifu Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. Neno: Maandiko Matakatifu Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. BIBLIA KISWAHILI Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. |
Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.
Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa kwenye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.
bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.
Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung'olewa kabisa;