Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mathayo 25:3 - Swahili Revised Union Version

Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mathayo 25:3
12 Marejeleo ya Msalaba  

Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.


Walakini wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki; hufurahi kumkaribia Mungu.


akiona upanga unakuja juu ya nchi hiyo, na kupiga tarumbeta na kuwaonya watu;


Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.


Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.


bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.


walio na utaua kwa nje, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.


mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.


Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.