Mathayo 21:14 - Swahili Revised Union Version Na vipofu na viwete wakamwendea mle hekaluni, akawaponya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Vipofu na vilema wengine walimwendea huko hekaluni, naye Yesu akawaponya. Biblia Habari Njema - BHND Vipofu na vilema wengine walimwendea huko hekaluni, naye Yesu akawaponya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Vipofu na vilema wengine walimwendea huko hekaluni, naye Yesu akawaponya. Neno: Bibilia Takatifu Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya. Neno: Maandiko Matakatifu Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya. BIBLIA KISWAHILI Na vipofu na viwete wakamwendea mle hekaluni, akawaponya. |
Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika,
Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huku na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.