Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; seuze nyumba hii niliyoijenga!
Mathayo 12:6 - Swahili Revised Union Version Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, nawaambieni kwamba hapa pana kikuu kuliko hekalu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, nawaambieni kwamba hapa pana kikuu kuliko hekalu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, nawaambieni kwamba hapa pana kikuu kuliko hekalu. Neno: Bibilia Takatifu Nawaambia wazi kwamba, yeye aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa. Neno: Maandiko Matakatifu Nawaambia wazi kwamba, yeye aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa. BIBLIA KISWAHILI Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. |
Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; seuze nyumba hii niliyoijenga!
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijia katika hekalu lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi.
Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato pasipo kupata hatia?