Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi.
Mathayo 1:17 - Swahili Revised Union Version Basi vizazi vyote tangu Abrahamu hadi Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hadi ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hadi Kristo ni vizazi kumi na vinne. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo. Biblia Habari Njema - BHND Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo, kulikuwa na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Ibrahimu hadi Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho wa Babeli hadi Al-Masihi. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo, kulikuwepo na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Ibrahimu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli hadi Al-Masihi. BIBLIA KISWAHILI Basi vizazi vyote tangu Abrahamu hadi Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hadi ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hadi Kristo ni vizazi kumi na vinne. |
Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi.
ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, hakuvichukua, hapo alipomchukua Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, toka Yerusalemu mpaka Babeli, pamoja na wakuu wote wa Yuda, na Yerusalemu;
Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,
Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).