Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika, Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake.
Matendo 8:23 - Swahili Revised Union Version Kwa maana nakuona uko katika uchungu kama nyongo, na tena uko katika kifungo cha uovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na u mfungwa wa dhambi!” Biblia Habari Njema - BHND Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na u mfungwa wa dhambi!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na u mfungwa wa dhambi!” Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana ninaona kwamba wewe umejawa na uchungu na ni mfungwa wa dhambi.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana ninaona kwamba wewe umejawa na uchungu na ni mfungwa wa dhambi.” BIBLIA KISWAHILI Kwa maana nakuona uko katika uchungu kama nyongo, na tena uko katika kifungo cha uovu. |
Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika, Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake.
Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu.
Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, BWANA wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.
Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
Njia yako na matendo yako yamekupatia haya; huu ndio uovu wako; kwa maana ni uchungu, hakika unafikia hata moyo wako.
Basi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji yenye sumu wayanywe.
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matusi yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;
Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.
mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.
Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;