Matendo 5:19 - Swahili Revised Union Version lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini usiku malaika wa Bwana aliifungua milango ya gereza, akawatoa nje, akawaambia, Biblia Habari Njema - BHND Lakini usiku malaika wa Bwana aliifungua milango ya gereza, akawatoa nje, akawaambia, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini usiku malaika wa Bwana aliifungua milango ya gereza, akawatoa nje, akawaambia, Neno: Bibilia Takatifu Lakini wakati wa usiku, malaika wa Mwenyezi Mungu akaja, akafungua milango ya gereza na akawatoa nje. Akawaambia, Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wakati wa usiku, malaika wa Mwenyezi Mungu akaja, akafungua milango ya gereza na akawatoa nje. Akawaambia, BIBLIA KISWAHILI lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, |
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Nebukadneza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.
Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;
Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hadi nitakapokuambia; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.
Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.
Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!
Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.
Ghafla pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.
Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami,
Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile iteremkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.