Kisha Paulo na wenziwe wakang'oa nanga wakasafiri kutoka Pafo, wakafika Perge katika Pamfilia. Yohana akawaacha akarejea Yerusalemu.
Matendo 27:5 - Swahili Revised Union Version Tulipopita bahari ya upande wa Kilikia na Pamfilia, tukafika Mira, mji wa Likia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Halafu tulivuka bahari ya Kilikia na Pamfulia, tukatia nanga Mura, mji wa Lukia. Biblia Habari Njema - BHND Halafu tulivuka bahari ya Kilikia na Pamfulia, tukatia nanga Mura, mji wa Lukia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Halafu tulivuka bahari ya Kilikia na Pamfulia, tukatia nanga Mura, mji wa Lukia. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya sisi kuvuka bahari iliyo upande wa Kilikia na Pamfilia, tukafika Mira huko Likia. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya sisi kuvuka bahari iliyoko upande wa Kilikia na Pamfilia, tukafika Mira huko Likia. BIBLIA KISWAHILI Tulipopita bahari ya upande wa Kilikia na Pamfilia, tukafika Mira, mji wa Likia. |
Kisha Paulo na wenziwe wakang'oa nanga wakasafiri kutoka Pafo, wakafika Perge katika Pamfilia. Yohana akawaacha akarejea Yerusalemu.
Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.
Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,
Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa.
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nilizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihada kubwa kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;
Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;