Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Matendo 15:41 - Swahili Revised Union Version Akapita katika Shamu na Kilikia akiyaimarisha makanisa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Katika safari hiyo alipitia Siria na Kilikia, akiyaimarisha makanisa. Biblia Habari Njema - BHND Katika safari hiyo alipitia Siria na Kilikia, akiyaimarisha makanisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Katika safari hiyo alipitia Siria na Kilikia, akiyaimarisha makanisa. Neno: Bibilia Takatifu Akapitia Siria na Kilikia, akiimarisha makundi ya waumini ya huko. Neno: Maandiko Matakatifu Akapitia Shamu na Kilikia, akiyaimarisha makundi ya waumini ya huko. BIBLIA KISWAHILI Akapita katika Shamu na Kilikia akiyaimarisha makanisa. |
Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu.
Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha.
Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Priskila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.
Na tulipoona Kipro tukaiacha upande wa kushoto; tukasafiri mpaka Shamu tukashuka Tiro. Kwa maana huko ndiko merikebu yetu itakakoshusha shehena yake.
Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;