Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
Matendo 11:3 - Swahili Revised Union Version wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Wewe umekwenda kukaa na watu wasiotahiriwa na hata umekula pamoja nao! Biblia Habari Njema - BHND “Wewe umekwenda kukaa na watu wasiotahiriwa na hata umekula pamoja nao! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Wewe umekwenda kukaa na watu wasiotahiriwa na hata umekula pamoja nao! Neno: Bibilia Takatifu wakisema, “Ulienda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao.” Neno: Maandiko Matakatifu wakisema, “Ulikwenda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao.” BIBLIA KISWAHILI wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. |
Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.
Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka.
Akawakaribisha wawe wageni wake. Hata siku ya pili, Petro akaondoka akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yafa wakafuatana naye.
Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali kwa mtu aliye Myahudi ashirikiane na mtu wa taifa lingine wala kumtembelea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu yeyote mchafu wala najisi.
Basi, tuma watu kwenda Yafa, ukamwite Simoni aitwaye Petro, anakaa katika nyumba ya Simoni, mtengenezaji wa ngozi, karibu na pwani; naye akija atasema nawe.
Lakini, mambo yalivyo, niliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
Kwa maana kabla hawajaja watu kadhaa waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini hao walipokuja, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.
Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.