Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Matendo 11:2 - Swahili Revised Union Version

Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye,

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Basi, Petro aliporudi Yerusalemu, wale Wayahudi waumini waliopendelea watu wa mataifa mengine watahiriwe, walimlaumu wakisema:

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Basi, Petro aliporudi Yerusalemu, wale Wayahudi waumini waliopendelea watu wa mataifa mengine watahiriwe, walimlaumu wakisema:

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Basi, Petro aliporudi Yerusalemu, wale Wayahudi waumini waliopendelea watu wa mataifa mengine watahiriwe, walimlaumu wakisema:

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hivyo Petro alipopanda Yerusalemu, waumini waliotahiriwa wakamshutumu,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hivyo Petro alipopanda Yerusalemu, wale wa tohara waliokuwa wameamini wakamshutumu,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye,

Tazama sura
Tafsiri zingine

Matendo 11:2
8 Marejeleo ya Msalaba  

Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.

Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;

Wakashuka watu waliotoka Yudea wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamuwezi kuokoka.

Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.

Na Yesu aitwaye Yusto awasalimu. Hao tu ndio watu wa tohara miongoni mwa wale watendao kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada kwangu.

Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao.