Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Matendo 10:19 - Swahili Revised Union Version

Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Petro alikuwa bado anajaribu kuelewa yale maono, na hapo Roho akamwambia, “Sikiliza! Kuna watu watatu hapa, wanakutafuta.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Petro alikuwa bado anajaribu kuelewa yale maono, na hapo Roho akamwambia, “Sikiliza! Kuna watu watatu hapa, wanakutafuta.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Petro alikuwa bado anajaribu kuelewa yale maono, na hapo Roho akamwambia, “Sikiliza! Kuna watu watatu hapa, wanakutafuta.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wakati Petro akiwa anafikiria kuhusu yale maono, Roho wa Mungu akamwambia, “Simoni, kuna watu watatu wanaokutafuta.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wakati Petro akiwa anafikiria juu ya yale maono, Roho wa Mwenyezi Mungu akamwambia, “Simoni, wako watu watatu wanaokutafuta.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Matendo 10:19
11 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.


wakaita; wakauliza kama Simoni aitwaye Petro anakaa humo.


Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!


Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;


Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.


Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.


Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia Paulo kwa uweza wa Roho asipande kwenda Yerusalemu.


Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukaribiane nalo.


lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.


Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;