Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Marko 9:48 - Swahili Revised Union Version ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Humo wadudu wake hawafi, na huo moto hauzimiki. Biblia Habari Njema - BHND Humo wadudu wake hawafi, na huo moto hauzimiki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Humo wadudu wake hawafi, na huo moto hauzimiki. Neno: Bibilia Takatifu Ni mahali ambako funza wao hawafi, wala moto wao hauzimiki. Neno: Maandiko Matakatifu mahali ambako “ ‘funza wake hawafi, wala moto wake hauzimiki.’ BIBLIA KISWAHILI ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. |
Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Jitahirini kwa BWANA, mkayaondoe magovi ya mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
ambaye ungo wake uko mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanja wake wa kupuria, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.