Maombolezo 3:44 - Swahili Revised Union Version Umejifunika nafsi yako kwa wingu, Maombi yetu yasipite. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Umejizungushia wingu zito, sala yeyote isiweze kupenya humo. Biblia Habari Njema - BHND Umejizungushia wingu zito, sala yeyote isiweze kupenya humo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Umejizungushia wingu zito, sala yeyote isiweze kupenya humo. Neno: Bibilia Takatifu Unajifunika mwenyewe kwa wingu, ili pasiwe na ombi litakaloweza kupenya. Neno: Maandiko Matakatifu Unajifunika mwenyewe kwa wingu, ili pasiwe na ombi litakaloweza kupenya. BIBLIA KISWAHILI Umejifunika nafsi yako kwa wingu, Maombi yetu yasipite. |
Ndipo BWANA akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.
Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni Kwa wingu katika hasira yake! Ameutupa toka mbinguni hata nchi Huo uzuri wa Israeli; Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake Katika siku ya hasira yake.
Ikawa kama wakati nilipowaita, wasitake kunisikiliza; basi, nao wataniita, wala sitasikiliza, asema BWANA wa majeshi.