Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu.
Luka 13:5 - Swahili Revised Union Version Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao.” Biblia Habari Njema - BHND Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao.” Neno: Bibilia Takatifu Nawaambia, la hasha! Ninyi nanyi msipotubu, wote mtaangamia vivyo hivyo.” Neno: Maandiko Matakatifu Nawaambia, la hasha! Ninyi nanyi msipotubu, wote mtaangamia vivyo hivyo.” BIBLIA KISWAHILI Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. |
Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu.
Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu?
Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.