Luka 11:8 - Swahili Revised Union Version Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa hatoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, atatoka na kumpa kadiri ya haja yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake, lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote anachohitaji. Biblia Habari Njema - BHND Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake, lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote anachohitaji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake, lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote anachohitaji. Neno: Bibilia Takatifu Nawaambia, ingawa huyo mtu hataamka na kumpa hiyo mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ya kuendelea kwake kuomba, ataamka na kumpa kiasi anachohitaji. Neno: Maandiko Matakatifu Nawaambia, ingawa huyo mtu hataamka na kumpa hiyo mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ya kuendelea kwake kuomba, ataamka na kumpa kiasi anachohitaji. BIBLIA KISWAHILI Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa hatoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, atatoka na kumpa kadiri ya haja yake. |
na yule wa ndani amjibu akisema, Usinisumbue; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kutoka nikupe?
Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu;
Maana nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili;
Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili msimame mkiwa wakamilifu na kuthibitika kabisa katika mapenzi yote ya Mungu.
Naye akalia mbele yake hizo siku saba, wakati ulioendelea karamu yao; basi ikawa siku ya saba akamwambia, kwa sababu alikuwa akimsisitiza sana; naye akawaambia wale wana wa watu wake hicho kitendawili.