Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma inakuzunguka, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.
Luka 11:12 - Swahili Revised Union Version Au akimwomba yai, atampa nge? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Na kama akimwomba yai, je, atampa nge? Biblia Habari Njema - BHND Na kama akimwomba yai, je, atampa nge? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Na kama akimwomba yai, je, atampa nge? Neno: Bibilia Takatifu Au mtoto akimwomba yai atampa nge? Neno: Maandiko Matakatifu Au mtoto akimwomba yai atampa nge? BIBLIA KISWAHILI Au akimwomba yai, atampa nge? |
Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma inakuzunguka, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.
Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au akimwomba samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.