Isaya 66:11 - Swahili Revised Union Version mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha, nanyi mtashiba kwa riziki zake; mtakunywa shibe yenu na kufurahi, kutokana na wingi wa fahari yake. Biblia Habari Njema - BHND Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha, nanyi mtashiba kwa riziki zake; mtakunywa shibe yenu na kufurahi, kutokana na wingi wa fahari yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha, nanyi mtashiba kwa riziki zake; mtakunywa shibe yenu na kufurahi, kutokana na wingi wa fahari yake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka katika faraja ya matiti yake; mtakunywa sana, na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka katika faraja ya matiti yake; mtakunywa sana, na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.” BIBLIA KISWAHILI mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukamua, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake. |
Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.
Utanyonya maziwa ya mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa Yakobo.
Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika makabila ya watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.
Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia.
Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA.
Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu.
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;