Isaya 50:5 - Swahili Revised Union Version Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bwana Mungu amenifanya msikivu, nami sikuwa mkaidi wala kugeuka mbali naye. Biblia Habari Njema - BHND Bwana Mungu amenifanya msikivu, nami sikuwa mkaidi wala kugeuka mbali naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bwana Mungu amenifanya msikivu, nami sikuwa mkaidi wala kugeuka mbali naye. Neno: Bibilia Takatifu Bwana Mungu Mwenyezi amezibua masikio yangu, nami sikuwa mwasi, wala sikurudi nyuma. Neno: Maandiko Matakatifu bwana Mwenyezi amezibua masikio yangu, nami sikuwa mwasi, wala sikurudi nyuma. BIBLIA KISWAHILI Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma. |
Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nilijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako;
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniondokee; lakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.
Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.
Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
Naye aliyenituma yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.
tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.